Mwanga wa kurejea La Liga, makundi ya wachezaji 10 yaruhusiwa kuwa pamoja mazoezini

Ligi kuu ya Hispania La Liga imekusudia kuziruhusu timu kuanza mazoezi kwa makundi leo Jumatatu ambapo kabla ya mazoezi ya makundi kila mchezaji alikuwa anafanya peke yake.

Wachezaji hupimwa virusi vya Corona kabla ya kuendelea kwa mazoezi ya mmoja mmoja ambapo tayari wachezaji watano wamebainika kuwa na Covid-19 katika ligi ya daraja la pili, idadi ya wachezaji chini ya 10 inaruhusiwa kufanyiwa mazoezi kwa pamoja kuanzia leo Jumatatu.

Baada ya mazoezi ya makundi hatua itakayofuata ni kuanza mazoezi ya pamoja ambayo yatakuwa yanakaribisha kurudi kwa ligi Juni 12 bila uwepo wa mashabiki.

Kupungua kwa idadi ya maambukizi ya virusi vya Corona kunamaanisha hakutakuwa na ulazima wa wachezaji na makocha kukaa hotelini au kambini badala yake wapo huru hata kukaa nyumbani

Author: Bruce Amani

Share With Your Friends