Mwanzo mpya CAF, Motsepe achaguliwa kuwa rais mpya

Bilionea wa Afrika Kusini, Patrice Motsepe, amechaguliwa bila kupingwa kuwa rais mpya wa Shirikisho la Kandanda barani Afrika, CAF, kwenye mkutano mkuu wa uliofanyika leo nchini Morocco.

Uchaguzi wake unafuatia makubaliano yaliyosimamiwa na Rais wa Shirikisho la Soka Duniani, FIFA, Gianni Infantino, wiki moja iliyopita, ambayo yanawawezesha wapinzani watatu wa Motsepe kuteuliwa kushika nyadhifa za umakamu wa rais wa CAF.

Akizungumza baada ya kuchaguliwa kwake, Motsepe ametoa wito wa kufanya kazi pamoja ili kuupeleka mbele mchezo wa soka barani Afrika na ameahidi kurejesha mafanikio yaliyowahi kupatikana kwenye kandanda miaka iliyopita.

Motsepe, ambaye ni mfanyabishara mwenye mafanikio makubwa lakini asiye na uzoefu mkubwa katika kusimamia kandanda, atamrithi Ahmad Ahmad aliyechaguliwa kuingoza CAF miaka minne iliyopita, lakini akaondolewa kwa tuhuma za rushwa.

Author: Bruce Amani

Sharing is caring!

0Shares