Mwendwa Aleta Tumaini KPL, Sasa Ligi Kuu Mbioni Kuanza

90

Rais wa Shirikisho la Kandanda nchini Kenya KPL Nick Mwendwa ametoa tumaini jipya kwa mashabiki na wadau wa kandanda nchini humo kufuatia kutegua kitendawili kizito ambacho kilibakia kutolewa miji na kukosa majibu.

Kitendawili ambacho Mwendwa amekitegua ni juu ya ni lini Ligi Kuu nchini Kenya FKFPL itaanza sambamba na Ligi za chini ambazo hazijachezwa tangia kumalizika kwa msimu uliopita 2021/22.

Klabu hasa za KPL zimeendelea kujiandaa bila kujua ni lini Ligi itaanza kwani Kamati ya mpito ya FKFPL ilikuwa inaendelea kubadilisha tarehe ya kuanza kwa Ligi kila kunapoitwa leo.

Hata hivyo, muda mfupi baada ya kurejea ofisini Nick Mwendwa ambaye alisimamishwa kuwa Rais wa Kenya kutokana na tuhuma za rushwa na matumizi mabaya ya ofisi ameweka wazi juu ligi itaanza rasmi tarehe za mwanzoni wa mwezi Oktoba.

“Ligi itaanza mapema mwezi ujao. Napenda nizikumbushe klabu na wachezaji kuendelea kujiandaa kwani mashindano yote yataanza na utaratibu utaendelea kama kawaida”, alisema Mwendwa.

Author: Asifiwe Mbembela