Mwenyekiti Gor Mahia Awaomba Wachezaji Kutoishtaki Klabu Fifa

164

Mwenyekiti wa Gor Mahia Ambrose Rachier amewaomba wachezaji wa kikosi hicho kuacha kuripoti taarifa Fifa za kutolipwa mshahara kwani klabu haifanyi hivyo kwa makusudi bali ni anguko la uchumi ambalo wanakabiliana nalo kwa sasa.

Kwa mjibu wa Mwenyekiti Rachier amesema K’Ogalo inapitia wakati mgumu kutokana na athari za Corona hata hivyo wanakabiliwa na kifungo cha kutosajili mpaka Januari 2023, endapo hili litafika mezani kwa Fifa kuna uwezekano wa kifungo kuongezwa.

Miongoni mwa wachezaji ambao walipeleka taarifa Fifa ni mchezaji wa zamani wa Singida United Shafik Batambuze, mchezaji wa zamani wa Dodoma Jiji FC Dickson Ambundo na Jackson Owusu.

“Tunakabiliwa na changamoto kadhaa ikiwemo ya uchumi ambayo ni kwa sababu ya Corona. Haijawai kuwa nia ya klabu kutaka kutowalipa mishahara wachezaji wetu, ni kitu ambacho kipo nje ya uwezo”, alisema Mwenyekiti huyo ambaye amekaa muda mrefu madarakani.

Author: Asifiwe Mbembela