Naibu Mwenyekiti wa Simba atamani makubwa Ligi ya Mabingwa Afrika

195

Wakati klabu ya Simba ikiwa imebakiwa na michezo miwili ya hatua ya makundi ya Ligi ya Mabingwa Afrika na kuhitaji alama moja pekee kufuzu kuingia hatua ya robo fainali ya Kombe hilo, Makamu Mwenyekiti wa Bodi ya Simba Salim Abdallah “Try Again” amejigamba kuwa wanataka makubwa zaidi kwenye mechi hizo mbili na sio alama moja pekee.

Simba itashuka dimba la Mkapa Jijini Dar Aprili 4 kucheza mechi dhidi ya AS Vita ya Congo ambapo wanahitaji alama moja tu kujikatia tiketi lakini Makamu Mwenyekiti Abdallah amesema wanahitaji ushindi kwenye huo mchezo ili kuvuna alama nne na sio moja.

Akizungumza karibuni na Wanahabari, Salim Abdallah “Try Again” amesema “Simba ni klabu kubwa hatutakiwi kuwa na malengo madogo, inatakiwa kuwa na malengo makubwa ili tujitengenezea mazingira ya kupangwa vizuri wakati wa droo” alisema.

Simba kwa sasa ina alama 10 ikishinda itafikisha alama 13 ambazo hazitaweza kufikiwa na timu yoyote na klabu inayofuatia ni Al Ahly ambayo ina pointi 7, AS Vita Club ina alama 4 na El Merriekh pointi moja mwishoni mwa kundi A.

Author: Asifiwe Mbembela