Mzee wa Kukera Morrison abeba tuzo Simba

Mzee wa Vituko aibuka shujaa akabidhiwa tuzo yake. Unamjua ni nani? Basi ni yule ambaye kwenye mechi ya Kombe la Shirikisho la TFF alifanya tukio kama lile alilofanya mchezaji mmoja wa Italia baada ya kushinda ubingwa wa Kombe la Dunia mwaka 2006 mbele ya Ufaransa.

Si mwingine bali ni mshambuliaji wa Simba raia wa Ghana, Bernard Morrison, ambaye leo amekabidhiwa kitita cha shilingi Milioni 1, kutoka kampuni ya Emirate Alluminium kufuatia kutwaa tuzo ya mchezaji bora wa Mwezi Juni.

Nyota huyo mzee wa kuchetua ametwaa tuzo hiyo baada ya kura za mashabiki kupigwa kwa wingi kupitia mitandao ya kijamii ambayo imechelewa kutolewa kutokana na kutokuwepo nchini kwa Morrison ambaye alikuwa Ghana kabla ya kwenda Kigoma.

Alitwaa tuzo huyo baada ya kuwashinda wachezaji wenzake ambao ni Luis Miquissone na nahodha wake John Bocco, ambapo walikuwa wakiwania tuzo hiyo pamoja.

Tuzo hiyo imekuwa ikitolewa na Kampuni ya Emirate Alluminum kila mwezi, huku mchakato wa kumpata mshindi huendeshwa na Simba kupitia kura za mashabiki wa klabu hiyo.

Author: Asifiwe Mbembela

Sharing is caring!

0Shares