Nahodha wa Watford Troy Deeney agoma kuanza mazoezi na wenzake kwa sababu ya Corona

Nahodha wa kikosi cha Watford Troy Deeney amesema hataanza mazoezi na wenzake kutokana na uwepo wa janga la Corona huku familia yake ikiwa katika hofu ya maambukizi.

Vilabu vya Ligi Kuu nchini England vimeanza rasmi Jumanne hii mazoezi katika makundi madogo madogo ili kuruhusu kurudi kwa Ligi lakini bado Troy aendelea kushikilia msimamo wake.

Deeney hataki kumweka mtoto wake kwenye hatari ya maambukizi, kwani ana tatizo katika mfumo wa upumuaji hivyo kuwa katika kundi la watu walio kwenye uwezekano mkubwa wa kupata virusi vya Corona.

“Tulitakiwa kurudi mazoezi wiki hii, lakini nimeshasema sitakwenda mazoezi” alisema mshambuliaji huyo mwenye miaka 31.

Watford bado hawajaanza mazoezi kama timu nyingine leo Jumanne ambapo wamekusudia kuanza rasmi kesho Jumatano, hata hivyo wamesema hawana tatizo na sababu ya kumzuia Deeney.

“Mtoto wangu ana miaka mitano tu, ana tatizo katika mfumo wa upumuaji, hivyo siwezi kurudi nyumbani kumuweka katika mazingira ya hatari kupata virusi hivyo”.

Deeney aliongeza kwa kusema kama watu hawajali juu ya taarifa zangu, kwa nini nitumie muda mwingi kuelezea hizo taarifa. “Sipo tayari kujiweka hatarini kwa ugonjwa huo”.

Tayari vilabu vimeanza mazoezi Jumanne hii, timu kama Liverpool, Wolves, Newcastle United zilionekana katika picha ya mazoezi licha ya kuendelea kuchukua tahadhari.

Author: Bruce Amani