Nairobi City Stars Yatoshana Nguvu na Sofapaka

51

Licha ya kutawala mchezo kwa muda mwingi, Nairobi City Stars wamelazimishwa sare ya bao 1-1 na Sofapaka katika mchezo wa Ligi Kuu nchini Kenya FKFPL mtanange uliopigwa dimba la Ruaraka Jumamosi ya Leo.

Walianza Simba wa Nairobi kufunga bao la kwanza kabla ya kikosi cha Sofapaka kusawazisha na kufanya mchezo huo kumalizika kwa sare ya goli hizo.

Wakati mchezo ukielekea ukingoni, Sofapaka walipata bao la kusawazisha baada ya Rody Manga kumalizia krosi ya Ben Stanley Omondi dakika ya 74 ya mchezo.

Baada ya mchezo huo, kocha wa Sofapaka David Ouma amewapongeza vijana wake kwa kuvuna alama moja wakati kocha wa City Stars akionyesha kutofurahishwa na sare hiyo.

Author: Asifiwe Mbembela