Namungo yamaliza safari ngumu ya Kombe la Shirikisho Afrika kwa vipigo

Namungo FC wamemaliza ratiba ya makundi ya Kombe la Shirikisho Afrika kwa aina yake, kufuatia kuhitimisha kabumbu hilo bila ushindi, bila goli la kufunga na kupoteza mechi zote, nyumbani na ugenini, jumla ya goli 9 imezipokea kutoka kwa timu tofauti.

Namungo ambao walikuwa kundi D pamoja na Raja Casablanca, Pyramids ya Misri, na Nkana FC, timu pekee ambazo zimeingia hatua ya robo fainali ni Pyramids na Raja Athletic.

Mchezo wa mwisho ulikuwa ni dhidi ya Pyramids uliochezwa Uwanja wa 30 June ambao ulisoma Pyramids 1-0 Namungo FC.

Bao pekee na la ushindi kwa Pyramids lilipachikwa wavuni na Ibrahim Adel dakika ya 65 na kuwapoteza jumlajumla wawakilishi wa Tanzania wanaonolewa na Hemed Morroco.

Ni Raja Casablanca yenye pointi 18 na Pyramids yenye pointi 12 zimetinga hatua inayofuata kutoka Kundi D, huku Nkana FC yenye pointi 6 na Namungo FC zikiishia katika hatua ya makun

Author: Asifiwe Mbembela

Sharing is caring!

0Shares