Namungo, Yanga hakuna mbabe

Kikosi cha Namungo Fc kimelazimishwa sare ya goli 1-1 na Yanga Sc katika mchezo wa Ligi Kuu Tanzania Bara mtanange uliopigwa dimba la Ilulu Mkoa wa Lindi leo Jumamosi Novemba 20, 2021.

Sare hiyo inaifanya kuwa ya sita kupatikana kwenye mechi ambazo zinaikutanisha Namungo na Yanga tangia mwaka 2019, iwe Dar es Salaam au Lindi.

Mabao kwenye mechi hiyo ambayo Yanga hakuwa kwenye ubora uliozoeleka kwenye mechi za Ligi msimu huu yamewekwa kimiani na Obrey Chirwa kwa shuti kali na lile bao la Saido Ntibazonkiza likiwa la penati baada ya Feisal Salum Fei Toto kufanyiwa faulo ndani ya eneo la hatari

Matokeo hayo yanaifanya Yanga kuendelea kuwa kileleni mwa msimamo wa Ligi Kuu nchini Tanzania Bara wakiwa na alama 16 wakati alama moja ya Namungo ikiwa chachu kwao.

Author: Asifiwe Mbembela

Share With Your Friends