Napoli wanabanwa mbavu na Barcelona Uefa

60

Barcelona imepata goli la ugenini katika mchezo wa Ligi ya Mabingwa Ulaya hatua ya 16 bora dhidi ya Napoli kwenye mtanange uliopigwa Italia ambapo mchezo umemalizika kwa sare ya goli 1-1.

Dries Mertens alikuwa wa kwanza kuipa uongozi Napoli kwa shuti kali la nje 18 katika ngwe ya kwanza na kufikia idadi ya goli 121 na kuwa miongoni mwa wachezaji wenye magoli mengi klabuni hapo sambamba na Marek Hamsik.

Mabingwa hao wa La Liga Barcelona walisawazisha kunako dakika ya 57 kupitia kwa Antoine Griezmann ambaye akimalizia pasi nzuri kutoka kwa Nelson Semedo.

Wageni pia walimaliza mtanange huo wakiwa pungufu kufuatia Arturo Vidal kuonyeshwa kadi nyekundu, hivyo Barcelona ambao ni vinara wa Ligi ya Hispania watakosa huduma ya Sergio Busquets ambaye pia ameonyeshwa kadi ya njano ya tatu msimu huu huku pia kukiwa na hatikati ya mlinzi Gerrard Pique

Author: Bruce Amani