Napoli yashindwa kupunguza mwanya dhidi ya Juventus

Napoli ilipoteza nafasi ya kupunguza mwanya kati yake na vinara wa ligi kuu ya kandanda Italia Juventus hadi pointi sita baada ya kukabwa kwa sare ya 0 – 0 na Fiorentina Jumamosi.

 

Juventus, ambayo ipo kwenye mkondo wa kuweka rekodi ya kutwaa ubingwa wa ligi kwa mara ya nane mfululizo, inaweza kutanua pengo hilo hadi pointi 11 kama itapata ushindi dhidi ya Sassuolo Jumapili.

 

Fiorentina imepungukiwa na pointi nne tu kufika nafasi za tiketi ya kucheza Europa League kabla ya kuchezwa mechi nyingine za ligi wikiendi hii.

 

Nambari tatu kwenye jedwali Inter Milan imepata pointi tatu baada ya ushindi wa 1 – 0 dhidi ya Parma. Sasa ina pointi 43 wakati Napoli ina 52. Bao la Inter limefugwa na Lautaro Martinez kunako dakika ya 79

Author: Bruce Amani

Share With Your Friends