NBC yaingia mkataba mnono wa EPL

Ligi Kuu nchini England imeingia kwenye mkataba na Kampuni ya NBC Universal wenye thamani ya pauni bilioni 2 kwa ajili ya kuonyesha mechi za mbashara za Ligi Kuu kwa miaka sita.

Kampuni hiyo yenye maskani yake nchini Marekani imekubali kuwa itaonyesha mechi zote za msimu kuanzia msimu ujao 2022/‪23-2027-2028‬ kwa walaji wa Marekani.

“Ni dili nzuri ambalo watu wa Marekani wameafikiana nasi, tunafurahi kuwa pamoja nao”, alisema Mkurugenzi Mtendaji wa EPL Richard Masters.

“Mkataba huu utafanya Ligi yetu kuwa maarufu nchini Marekani ambapo pia tunaamini NBC Sports watapata mrejesho mzuri”.

Umekuwa mwaka wa neema kwa Ligi Kuu England, itakumbukwa mwezi Mei 2021 iliingia mkataba na makampuni matatu ya nyumbani (England) Sky Sports, BT Sport, Amazon Prime Video na BBC Sport wenye thamani ya bilioni 4.7 kwa ajili ya kuonyesha mechi kwa walaji wa nyumbani.

Author: Asifiwe Mbembela

Share With Your Friends