Newcastle United Yanyunyiza Presha kwa Everton

181

Newcastle United imeibuka na ushindi mzito wa bao 4-1 dhidi ya Everton na kuendeleza presha kwa kocha Sean Dyche kwani sasa wako kwenye mstari wa kushuka daraja endapo wataendelea kutofanya vizuri.

Ushindi wa Newcastle umepatikana katika dimba la Goodison Park ambapo magoli yamefungwa na Callum Wilson aliyeingia kambani mara mbili, Joelinton, Jacob Murphy wakati bao la kufutia machozi limefungwa na Dwight McNeil.

Kwa matokeo hayo, Newcastle wanaendelea kushika nafasi ya tatu nyuma ya Manchester United katika nafasi ya nne, Everton wanashika nafasi ya 19 kwenye.

Author: Bruce Amani