Newcastle yamtimua kocha Steve Bruce

Newcastle United imefuta kazi aliyekuwa kocha wa kikosi hicho Steve Bruce baada ya makubaliano baina ya pande mbili, Bruce anaondoka siku 13 pekee tangia Newcastle kuingia mkataba na matajiri kutokea Saudi Arabia wenye thamani ya pauni milioni 305.

Kocha huyo mwenye umri wa miaka 60, alikiongoza kikosi cha Newcastle United katika mchezo wa 1,000 uliomalizika kwa kipigo cha goli 3-2 dhidi ya Tottenham Hotspur mtanange wa Jumapili.

Akizungumza baada ya mchezo, Bruce alisema katika kipindi chote akiwa Newcastle kulikuwa na milima na mabonde lakini anaamini ujio wa wawekezaji wapya kunaweza kuhamsha mafanikio.

Graeme Jones atachukua mikoba ya Steve Bruce kwa muda wakati Mwalimu wa muda mrefu akitafutwa.

Bruce anaondoka baada ya kukiongoza kikosi hicho kutoa sare tatu pekee kwenye mechi nane za Ligi, lakini anaondoka baada ya kuwa klabuni hapo tangia Julai 2019, miongoni mwa mafanikio ni pamoja na kumaliza nafasi ya 13, 12.

“Ninapenda kumshukuru kila mmoja ambaye anahusika na Newcastle United kwa namna moja au nyingine kuanzia wachezaji, makocha na viongozi kwa kunipa nafasi ya kuifundisha timu yenye historia ya namna yake”.

Author: Bruce Amani

Share With Your Friends