Neymar aifungia PSG lakini azomewa na mashabiki

Licha ya kufunga goli pekee na kuisaidia timu yake kunyakua alama tatu katika mchezo wa Ligi Kuu ya Ufaransa kwa PSG dhidi ya Strasbourg lakini bado mashabiki wa klabu hiyo wamemzomea mshambuliaji wa Kibrazil Neymar kwenye mchezo mzima.
Neymar akiwa amekosa mechi tano za mwanzo za PSG ikiwemo ya Ngao ya Hisani kutokana na shinikizo lake la kuhitaji kurejea kwenye kikosi cha FC Barcelona kabla ya kushindikana alifunga goli dakika za awali ingawa lilikataliwa kabla hajafunga kwenye muda wa lala salama.
Kwenye mechi hiyo pia, Ander Herrera(Manchester United), Mauro Icardi(Inter Milan) na mlinda mlango Navas (Real Madrid) wameonekana na kuwa sehemu ya mchezo wa leo
Hata hivyo, kurejea kwa Neymar hakuna maana kwenye Ligi ya Mabingwa kwani atakosa mechi tatu ikiwemo ya Real Madrid Jumatano baada ya kufungiwa msimu uliomalizika kwa kutoa maneno yaliyo tafsiriwa kama kejeli kwa shirikisho la Uefa baada ya mchezo wa PSG na Manchester United.

Author: Bruce Amani

Share With Your Friends