Neymar aisaidia PSG kuendeleza ubabe Ligi ya Ufaransa

Matajiri wa Paris St-Germain wameendeleza ubabe wao kwenye ligi Kuu nchini Ufaransa baada ya kushinda goli 1-0 dhidi ya Lyon, ushindi unaoifanya kuwa mbele alama tatu zaidi ya timu iliyo katika nafasi ya pili kwenye michezo 6.

Ushindi huo umeletwa na mshambuliaji wa Kibrazil Neymar akitumia ubunifu wa hali ya juu kuipita ngome ya Lyon kabla ya kushinda goli hilo kunako dakika ya 87.

Neymar kwenye mchezo uliopita alizomewa na mashabiki wake kabla ya kufunga goli la ushindi dakika ya 92 dhidi ya Strasbourg wikendi iliyopita.

Akiwa amekosa mechi tano za awali za PSG kipindi anajaribu kurudi Barcelona kurejea kwake kumeongeza kitu, mpaka sasa amefunga goli mbili kwenye mechi mbili alizocheza.

Mpaka sasa, PSG anaongoza Ligue 1 akiwa na pointi 15 michezo sita wakati Angers na Nice zikishika nafasi ya pili na tatu.

Author: Bruce Amani

Share With Your Friends