Neymar atupwa nje, PSG ikichapwa 1-0 na Lille Ligue 1

Lille inayoshiriki Ligi Kuu nchini Ufaransa Ligue 1 imefanikiwa kuwatandika mabingwa watetezi wa Ligi hiyo Paris St-Germain kwa goli 1-0 katika mchezo uliopigwa Leo Jumamosi Aprili 3.

Wakati Lille wakishinda na kwenda kileleni kwa Ligi hiyo kwa tofauti ya alama tatu, mshambuliaji wa Kibrazil Neymar Jr alionyeshwa kadi nyekundu kufuatia kadi mbili za njano sawa na mchezaji mwingine wa Lille.

Hata hivyo bao la Jonathan David liliwapa uongozi Lille ambalo lilidumu kwa dakika zote tisini.

Mabingwa watetezi hao wanahitaji taji la nne mfululizo la Ligue 1 ingawa kwa mwaka huu inaonekana kuwa ngumu, na mara ya mwisho kwa Lille kushinda taji la Ligi Kuu ilikuwa mwaka 2010/11.

PSG, wanafikisha mechi 10 msimu huu za kupoteza mashindano yote, mechi ijayo itakuwa dhidi ya Bayern Munich robo fainali ya Ligi ya Mabingwa Ulaya Jumatano hii.

Author: Asifiwe Mbembela

Sharing is caring!

0Shares