‘Ni wakati wa mabadiliko’ Yaya Toure amuunga Drogba kupata urais wa chama cha soka Ivory Coast

Kiungo wa zamani wa Ivory Coast Yaya Toure ameonyesha wazi mapenzi yake kwa aliyekuwa nahodha na mchezaji mweza Didier Drogba baada ya kusema atampigia kura katika kinyang’anyiro cha Urais wa Chama cha kandanda cha taifa hilo.

Drogba ameamua kugombea nafasi ya Rais ndani ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Ivory Coast (FIF) uchaguzi ambao mpaka sasa haujaweka tarehe rasmi ya kufanyika kwake kutokana na uwepo wa COVID-19.

“Ni wakati wa mabadiliko katika mpira wetu. Tunahitaji kuufanya mpira wetu kuwa wa kisasa”, alisema Toure.

“Ninaposema niko upande wa Drogba, ni kwa mazuri ya nchi yetu, kuwa na mchezaji mwenye mapenzi ya hivi na amewekeza Afrika litakuwa jambo la heri kwetu.”

Drogba kabla ya kustaafu alichezea mechi 105 za taifa lake, atakutana na changamoto kubwa kutoka kwa Rais wa sasa Sory Diabate na Makamu Rais wa FIF Idriss Diallo.

Hata hivyo, licha ya sapoti ya Toure, Umoja wachezaji wa soka nchini humo wanampinga Drogba na wanaonyesha mapenzi kwa Rais aliyepo madarakani Diabete.

Author: Bruce Amani

Share With Your Friends