Nice wapigwa STOP mashabiki kuingia uwanjani

Klabu ya Nice italazimika kucheza mechi zake za nyumbani bila mashabiki kutokana na mchezo wao dhidi ya Marseille Jumapili kusitishwa baada ya mashabiki kuvamia uwanjani, kwa maana hiyo mtanange dhidi ya Bordeaux utapigwa bila mashabiki.

Mbali na Nice, Mtaalamu wa viungo wa Marseille Pablo Fernandez amepigwa rungu kutokana na vitendo visivyokuwa vya kimichezo katika mchezo huo wa Jumapili.

Kama ulikuwa hujui, ilikuwa hivi; winga wa zamani West Ham United na sasa Marseille Dimitri Payet akienda kupiga kona kabla ya kupigwa na kopo kisha akalichukua kopo hilo na kulirusha walikokuwa wamekaa mashabiki wa Nice, hasira ya mashabiki ikapanda na kuvamia uwanjani.

Vurugu hizo zilizuiliwa na walinzi wa uwanjani pamoja na wachezaji lakini ilikuwa mgumu, na mchezo huo kulazimika kuota mbawa.

Baada ya muda vurugu kuisha, wachezaji wa Nice waliokuwa wanaongoza goli 1-0, walirejea uwanjani lakini wale wa Marseille walikataa.

Timu zote mbili zimepelekwa kwenye vyombo vya mpira vya kisheria.

Author: Bruce Amani

Sharing is caring!

0Shares