Nigeria atautafuna mfupa ulioishinda Misri?

Afrika Kusini baada ya kuiondosha timu mwenyeji Misri hatua ya 16 bora leo Jumatano Julai 10 itaingia katika dimba la Kimataifa la Cairo dhidi ya Nigeria hatua ya robo fainali ya michuano ya Kombe la Mataifa Afrika 2019.

Afrika Kusini ikiwa na kiwango finyu kwenye makundi baada ya kupoteza mechi mbili na ushindi mmoja kisha ushindi dhidi ya Mapharao Misri kwa goli 1-0 unaifanya timu hiyo kupata ari mpya ya kupambana kuelekea mchezo leo.

Nigeria ilipata ushindi muhimu hatua ya 16 bora dhidi ya Mabingwa watetezi wa Kombe hilo Cameroon kwa goli 3-2 huku pia hatua ya makundi ikimaliza nafasi ya pili juu ya Madagascar kwa kufikisha alama 6.

REKODI ZA HIVI KARIBUNI ZA AFCON

10.02.2000 Jijini la Lagos (Nusu Fainali) Nigeria 2-0 Afrika Kusini

31.01.2004 Mchezo wa hatua ya makundi Nigeria 4-0 Afrika Kusini

Mshindi wa mchezo kati ya Nigeria dhidi ya Afrika Kusini atakutana na mbabe kati ya Ivory Coast au Algeria hatua ya nusu fainali.

Author: Bruce Amani

Facebook Comments