Nigeria ya kwanza kutinga hatua ya timu 16 za mwisho

45
Nigeria imekuwa timu ya kwanza kufuzu hatua ya 16 bora kwa michuano ya Kimataifa Afrika 2019 nchini Misri baada ya kuitungua Guinea kwa goli 1-0 katika mchezo uliochezwa leo Jumatano.
Ushindi wa Nigeria “Super Eagles” umepatikana kupitia goli maridadi la kichwa la mlinzi Kenneth Omeruo lililodumu kwa mda wa dakika 90.
Mbali na kuwa na staa Naby Keita Guinea haikufua dafu mbele ya mastaa kama Iwobi, Obi na wengine. Michezo itakayoamua nani anaungana na Nigeria ni kati ya Madagascar dhidi ya Burundi siku ya Alhamisi hii, pamoja na michezo ya kukamilisha raundi zote tatu kwa michuano ya AFCON 2019.

Author: Bruce Amani