Nigeria yafanya mazoezi gizani wakijiandaa kuwavaa Benin mechi ya kufuzu Afcon 2021

297

Timu ya Taifa ya Nigeria Super Eagles imelazimika kufanya mazoezi kwenye uwanja wa Stade Charles de Gaulle, mjini Porto-Novo huku kukiwa na giza, yakiwa ni mazoezi ya kujiandaa na mchezo wa kufuzu Kombe la Mataifa Bingwa Afrika Afcon 2021 dhidi ya Benin.

Kwa mujibu wa vyanzo mbalimbali ni kuwa Maofisa wa uwanja huo, walizima taa zote huku Waandishi wa Habari kutoka Nigeria pia wakikatazwa kuingia viwanjani.

Vijana hao wa Super Eagles wamepangwa kucheza na Benin leo Jumamosi Machi 27 dimba la Stade Charles de Gaulle, hapo hapo mjini Porto-Novo.

Hata hivyo, Nigeria ndiyo vinara wa kundi L wakiwa na alama nane baada ya raundi nne wakati Benin wakishika nafasi ya pili na alama saba.

Matokeo ya sare yatawafanya Nigeria kufuzu kuingia kwenye fainali ya Kombe la Mataifa Bingwa Afrika Afcon 2021 Cameroon.

Author: Bruce Amani