Nigeria yaivunja mioyo ya Waafrika Kusini

Nigeria wamefanikiwa kuutafuna mfupa uliomshinda Misri baada ya leo Jumatano kupata goli 2-1 dhidi ya mfupa huo Afrika Kusini Bafana Bafana katika mtanange uliopigwa dimba la Kimataifa Cairo na kufuzu hatua ya nusu fainali ya mashindano ya Afcon 2019 nchini Misri.

Super Eagles inakuwa timu ya pili kufuzu nusu fainali baada ya kutanguliwa kwa Simba wa Teranga Senegal kwa kuifunga Benin goli 1-0 na kutinga hatua hiyo.

Winga wa Villarreal ya Hispania Samuel Chukwueze alifungua akaunti ya magoli kwa Nigeria dakika ya 27 akipokea mgongeo wa Alexis Iwobi kabla ya dakika ya 77 Afrika Kusini kupata goli lililofungwa na Bongani Zungu, dakika moja kabla ya mpira kumalizika Nigeria wakaongeza goli kwenye akaunti yao kupitia kwa William Troost Ekong.

Afrika Kusini wanaondoka Cairo Misri kwa amani baada ya kuiondosha Misri wenyeji na kufuzu hatua ya 16 bora kupitia kundi lililokuwa likitajwa kuwa ni la kifo.

Super Eagles Nigeria watakuna na mshindi kati ya Ivory Coast ama Algeria mchezo utakaochezwa dimba la Suez saa 1 usiku Alhamis.

Author: Bruce Amani

Facebook Comments