“Nilikataa kurejea Barcelona kama kocha kazi ilikuja mapema mno”- Xavi

55

Wiki hii ilivuma mitandao taarifa iliyokuwa inamhusisha kiungo mkabaji Xavi kurejea Barcelona kwa mara pili katika majukumu tofauti na sasa ilikuwa Ukocha.

Taarifa hiyo ilikuja baada ya Barca kumtimua aliyekuwa kocha wao Valverde kisha wakampa kipaumbele Xavi kuwa meneja mpya lakini kiungo huyo aliamua kuipiga chini ofa ya Wacatalunya hao. Je unaijua sababu ya kushindwa kujiunga na Fc Barcelona? Hii hapa..

“Nilikataa kwa sababu ofa hiyo ilikuja mapema mno kwangu”.

Kiungo huyo wa zamani wa Hispania amekuwa kocha wa Al Sadd tangu alipostaafu kucheza mpira wa ushindani kwenye klabu ya Qatari mwezi Mei mwaka jana.

Mkurugenzi mkuu wa Barcelona Oscar Grau na Mkurugenzi wa klabu hiyo Eric Abidal baada ya kufikia makubaliano ya kuvunja mkataba na Ernesto Valverde walimpa Xavi ofa ya kukinoa kikosi cha Barca kabla ya kuipiga chini.

Akizungumzia kuhusu kukataa ofa hiyo, Xavi alisema “Sikukubali kwa sababu ilikuwa mapema sana lakini bado inasalia kuwa ndoto yangu ya kuinoa timu niipendayo(Barca).” Alisema Xavi, 39.

Xavi, akiwa Barcelona alicheza michezo 750 kuanzia mwaka 1998 mpaka 2015 alipoulizwa kuhusu kocha mpya Quique Setien alisema anampenda kulingana na kazi anayoifanya.

Author: Bruce Amani