Nini kitafanyika kama timu ya England itashinda Champions League?

54

Kwa sababu Spurs au Liverpool inaweza kuwa bingwa wa Ulaya ni timu nne pekee za England zinazoingia katika Champions League msimu ujao – mradi tu Spurs pia itamaliza katika nne bora kwenye ligi.

Nafasi ya “ziada” ya hatua ya makundi itawaendea mabingwa wa Austria, ambao wangelazimika kufuzu kupitia mechi za mchujo kwa sababu ni ligi inayoorodheshwa nambari 11 kwa viwango vya Uefa.

Hata hivyo, kama timu ya England itabeba Kombe la Champions League na kumaliza nje ya nne bora katika Ligi ya Premier – uwezekano kwa Spurs – basi timu tano za England zitatinga hatua ya makundi msimu ujao

Hakuna nafasi ya Champions League kwa timu inayoshindwa katika fainali. Liverpool haingefuzu mwaka huu kama haingemaliza katika nne bora msimu wa 2017-18

Uefa ilibadilisha kanuni za kufuzu mwaka jana – kwa kuanza na mashindano ya msimu huu.

Mwaka wa 2012 Tottenham ilimaliza nafasi ya nne lakini ikapoteza nafasi ya kucheza Champions League kwa sababu Chelsea ilibeba Kombe hilo – lakini Spurs ingefuzu chini ya kanuni za sasa.

Hadi mwaka wa 2005, washindi wa Champions League hawakuwa wakifuzu moja kwa moja – kanuni iliyobadilishwa wakati Liverpool ilishinda Kombe hilo lakini haikumaliza katika nne bora.

Author: Bruce Amani