Nuno Espirito Santo ataka mazungumzo na Harry Kane, Spurs

Kocha wa Tottenham Nuno Espirito Santo amesema kuwa hajazungumza bado na mshambuliaji wake Harry Kane licha ya mchezaji huyo kuhusishwa kuondoka klabuni hapo.

Nuno Espirito Santo ameyasema hayo baada ya mchezo wa kirafiki dhidi ya Chelsea na kumalizika kwa sare ya bao 2-2, huku Harry Kane akiwa hajajitokeza mazoezi wiki hii ambayo alitakiwa kufika

“Kweli nahitaji kuzungumza na Harry. Bado sijapata nafasi”, alisema Nuno ambaye amekuwa kocha wa Spurs kuanzia majira ya kiangazi akitokea Wolves.

Kocha huyo amesisitiza kuwa anahitaji kuzungumza naye ndani sio kila mmoja kujua, ingawa kwa sasa akili ya mchezaji huyo ni kwenda Etihad Man City, tayari anahusishwa akiwa na takwimu za kutosha, amefunga goli 221.

Katika mchezo huo wa kirafiki, magoli ya Chelsea ambayo ilitangulia kuingia kambani yalifungwa na Hakim Ziyech wakati Spurs waliibuka kupitia kwa Lucas Moura na Steven Bergwin.

Author: Bruce Amani

Share With Your Friends