Nyota bora yaendelea kwa Ruben Dias ashinda tuzo ya Mchezaji Bora EPL, Guardiola amfunika Solskjaer

Beki wa kati wa Manchester City Ruben Dias ametwaa tuzo ya mchezaji bora wa Ligi Kuu England huku kocha wa klabu hiyo Pep Guardiola akitwaa pia tuzo.
Dias raia wa Ureno mwenye umri wa miaka 24, tangia usajili wake kunako klabu ya Manchester City akitokea Benfica kwa ada ya pauni milioni 65 aligeuka nuru na kuisaidia Man City kutwaa ubingwa wa tatu katika miaka minne.
Ni kama nyota njema kwake, kwani mwezi Mei mchezaji huyo alishinda pia tuzo ya mchezaji bora kupitia Chama cha Waandishi wa Habari Uingereza.
Bosi wa City Guardiola ametajwa kuwa kocha bora.
Goli la aina yake (rabona) lililofungwa na kiungo mshambuliaji wa Tottenham Eric Lamela dhidi ya Arsenal katika dabi ya London limetwaa goli bora la Msimu.
Tuzo ya Diaz inamaanisha kuwa amewashinda washindani wake ambao ni kiungo wa Manchester United Bruno Fernandes, Kelvin de Bruyne, Harry Kane, Mohamed Salah, Mason Mount, Jack Grealish, Thomas Soucer wa West Ham United.
Wakati Pep Guardiola amewashinda wapinzani wake ambao ni kocha wa Manchester United Ole Gunnar Solskjaer, Brendan Rodgers, David Moyes pamoja na yule wa Leeds United Marcelo Bielsa.

Author: Bruce Amani

Sharing is caring!

0Shares