Nyota Oburu Ang’aa Ligi ya Zambia

254

Nyota wa kimataifa wa Kenya Vincent Oburu anayekipiga kunako klabu ya Zesco United amechaguliwa kuwa mchezaji bora wa mchezo wa Ligi Kuu nchini Zambia baada ya kufunga goli moja na kutoa asisti katika goli lingine kwenye mechi iliyomalizika kwa matokeo ya 2-1, dhidi ya Nkaka FC.

Oburu ambaye ni mchezaji wa zamani wa Wazito FC alikuwa kwenye ubora mkubwa ambapo pengine kama angekuwa makini zaidi angeweza hata kufunga goli zaidi ya hilo moja, uzuri ameisaidia timu yake kuvuna alama zote tatu.

Oburu alifunga goli kunako dakika ya 21 dakika tatu baadaye wageni Nkana walipata goli moja kupitia kwa David Obashi aliyefunga kwa njia ya penati hata hivyo John Ching’adu aliipa Zesco ushindi mjarabu akiwa nahodha wa timu hiyo.

Nyota Oburu alikatisha mkataba na Wazito kabla ya kuibukia kunako klabu hiyo yenye maskani yake huko Zambia.

Author: Bruce Amani