Nyota wa Barcelona na Liverpool Javier Mascherano atangaza kustaafu

Kiungo mkabaji wa zamani wa Barcelona na Liverpool Javier Mascherano ametangaza rasmi kustaafu kucheza soka la ushindani baada ya kuitumikia kandanda kwa muda mrefu. Kiungo huyo mwenye umri wa miaka 36 alikuwa anachezea katika klabu ya Estudiantes nchini Argentina ambako ndiko nyumbani.

Akitangaza kustaafu tayari ni mshindi wa Ligi ya Mabingwa Ulaya mara mbili, La Liga mara tano kwenye miaka nane aliyokuwa Camp Nou. “Natangaza rasmi kustaafu kwenye taaluma yangu ya soka. Naishukuru sana klabu hii ambayo ilinipa nafasi ya kumalizia taaluma hapa” alisema Javier Jana Jumapili.

Mascherano ameitumikia mechi 147 Timu ya taifa ya Argentina na alianza kucheza soka lake katika klabu ya River Plate. Alicheza West Ham mwaka 2006 – 2007, akajiunga na Liverpool hadi mwaka 2010 ambapo alitua Barcelona na kucheza kuanzia mwaka 2010-2018.

Author: Bruce Amani