Nyota wa Liverpool Salah akutwa tena na maambukizi ya Covid-19

Staa wa Liverpool Mohamed Salah amekutwa tena na maambukizi ya virusi vya Corona ikiwa ni mara ya pili ndani ya wiki mbili kwenye majukumu ya timu ya taifa ya Misri. Salah, 28, wiki iliyopita alipimwa na kukutwa na dalili za Covid-19 leo tena Jumatano mamlaka za soka nchini Misri zimesema amekutwa na maambukizi yasiyoonyesha dalili.

Kwa hali hii, huenda akakosa mechi mbili za Liverpool kwa sababu atalazimika kujitenga mwenyewe kwa angalau siku 10. Liverpool watacheza na Leicester City mchezo wa Ligi Jumapili kabla ya kumenyana na Atalanta katika mbilinge mbilinge za Ligi ya Mabingwa Ulaya Novemba 25.

Author: Bruce Amani