Nyota wa Nigeria ajiunga na Brentford ya England

Brentford imekamilisha uhamisho wa mchezaji wa kwanza baada ya kupanda Ligi Kuu England, usajili huo ni wa nyota wa kimataifa wa Nigeria, anayefahamika kwa jina la Frank Onyeka kutokea klabu ya FC Midtjylland amemwaga wino.

 

Mchezaji huyo wa nafasi ya kiungo anajiunga na Brentford kwa kandarasi ya miaka mitano ambapo, fedha za usajili imefanywa kuwa siri.

 

Onyeka, 23, baada ya kujiunga na timu hiyo Jumatatu alisema atajitenga mwenyewe kwa angalau siku 14 kabla ya kujiunga na wenzake mazoezi ambao sasa wanaendelea na mazoezi ya kujiandaa na msimu ujao 2021/22.

 

“Tunafikiria kuwa atakuwa ingizo nzuri kwetu,” Alisema kocha Thomas Frank.

 

Brentford watacheza EPL msimu ujao kufuatia kuwa nje kwa takribani miaka 74, walipata nafasi hiyo kwa ushindi wa goli 2-0 dhidi ya Swansea City katika mchezo wa mtoano.

 

Onyeka mpaka sasa amecheza mechi moja pekee ngazi ya taifa lake la Nigeria ingawa anaweza akateuliwa kwenye Afcon ya mwaka 2022.

Author: Bruce Amani

Sharing is caring!

0Shares