Nyota wa zamani wa Chelsea Shevchenko abwaga manyanga Ukraine

409

Mshambuliaji wa zamani wa Chelsea Andriy Shevchenko ameachana rasmi na kazi ya ukocha katika Timu ya Taifa ya Ukraine licha ya matokeo mazuri kwenye michuano ya Euro 2020.

Shevchenko, 44, aliteuliwa kuwa kocha wa Ukraine mwaka 2016 ambapo amekiongoza kikosi hicho kufika hatua ya robo fainali ya Euro 2020 kabla ya kufungwa 4-0 na England mjini Rome.

“Kwa pamoja tulionyesha namna mchezo unaweza kuwa wa ushindani, wenye kuzalisha na sehemu ya furaha na mapumziko”, alisema kupitia mtandao wake wa Instagram.

Shevchenko, aliachana na soka la ushindani mwaka 2012, anaendelea kubakia kuwa mshambuliaji mwenye goli nyingi timu ya taifa ya Ukraine akiwa na bao 48 katika mechi 111.

Author: Bruce Amani