Ofa ya Man United kwa Sancho yapigwa chini na Dortmund

Ofa ya Manchester United kwenda kwa winga wa kimataifa wa England na Borrusia Dortmund Jadon Sancho ya pauni milioni 67 imepigwa chini ya klabu hiyo ya Ujerumani.

Klabu ya Dortmund imesema inahitaji kiasi cha pauni milioni 77.5 kwa Sancho mwenye umri wa miaka 21 kukiwa na ongezeko la kiasi cha pauni milioni 4.25 kama bonasi.

Inaelezwa kuwa Manchester United walipanga kukubali dau hilo la pauni milioni 77 kwa kulilipa kwa muda wa miaka mitano lakini Dortmund wakaongeza bonasi hiyo kufikia nne kabla ya hapo ilikuwa haifikii.

United sasa wanategemewa kutuma tena ofa nyingine kwa nyota huyo ambaye msimu uliopita pia alishindwa kutua Old Trafford.

Kocha Ole Gunnar Solskjaer amepanga dili hilo kukamilika kabla ya kuanza kwa maandalizi ya msimu ujao ambapo amemtaja mchezaji huyo kama kipaumbele chake.

Author: Asifiwe Mbembela

Sharing is caring!

0Shares