Ole apewa mktaba wa kudumu na Manchester United

Habari nzuri mchana huu kwa mashabiki wa Manchester United. Ujumbe ambao wamekuwa wakisubiri kuusikia hatimaye umetolewa. Manchester United imethibitisha kuwa imempa mkataba wa kudumu kocha Ole Gunnar Solskjaer. Man Utd imeshinda mechi 10 kati ya 13 za Premier tangu Mnorway Ole Gunnar Solskjaer alipowasili Desemba 19, 2018.

“Hiin ndio kazi ambayo kila wakati niliota kuifanya na nimefurahi sana kupata nafasi ya kuongoza timu hii kwa kipindi kirefu na natumai kuendelea kuleta mafanikio ambayo mashabiki wetu wazuri wanastahili.”

Raia huyo wa Norway, 45, aliwasili katika uwanja wa Old Trafford kama kaimu kocha Desemba ili kujaza pengo la Jose Mourinho.

Solskjaer alihudumu misimu 11 kama mchezaji wa United akifunga mabao 126 katika mechi 366 likewmo goli la ushindi katika fainali ya vilabu bingwa Ulaya 1999.

Kumekuwa na majina ya makocha ambao wangeweza kuchukua nafasi ya kocha wa kudumu na jina la kocha wa Spurs Mauricio Pochetino lilitajwa sana

Author: Bruce Amani

Share With Your Friends