Ole Gunnar Solskjaer amsifia Paul Pogba kwa kuimarika kiakili

122

Kocha wa Manchester United Ole Gunnar Solskjaer ametoa pongezi kwa kiungo wake mshambuliaji raia wa Ufaransa Paul Pogba licha ya kufanya makosa yaliyopelekea kipigo cha Arsenal kwa klabu hiyo. Solskjaer amesema Pogba amekuwa huru kiakili baada ya tukio lile jambo linalomfanya awe kwenye uwezekano wa kumtumia katika mchezo ujao wa timu hiyo wa Ligi ya Mabingwa Ulaya.

Pogba, 27, alisababisha tuta katika ushindi wa goli 1-0 waliouoata The Gunners siku ya Jumapili kwa kumuangusha beki wa Arsenal Hector Bellerin.

“Paul alijua kabisa ana uwezo wa kuucheza ule mpira lakini hata aliposhinda alionekana akinyosha mikono” alisema Solskjaer. Pogba msimu huu ameshacheza mechi tisa ndani ya uzi wa Manchester United ingawa msimu uliopita ulikuwa mgumu zaidi kwake akiutumia zaidi katika vitanda vya madaktari.

Kocha Ole anaweza kumpumzisha kiungo wake na kumtumia kiungo wa kidachi Donny van de Beek katika mtanange wa kesho Jumatano dhidi ya Istanbul Basaksehir.

Itakumbukwa mara baada ya mchezo, Pogba aliomba radhi kwa tukio lile akizungumza na Waandishi wa Habari.

Author: Asifiwe Mbembela