Omala Amuibua Kocha McKinstry wa Gor Mahia

207

Kocha Mkuu wa Gor Mahia Johnathan McKinstry amemtia moyo mshambuliaji wake Benson Omala kuwa atakuwa na kesho nzuri ngazi klabu na timu ya taifa licha ya mchezaji huyo kinara wa kupachika mabao KPL kutojumuishwa kwenye kikosi cha wachezaji 24 wanaounda Harambee Stars.

Omala mwenye bao 19 kwenye mechi 20 msimu huu wa mashindano ndani ya Gor Mahia hajajumuishwa kwenye kikosi cha Kenya ambacho kitacheza mechi ya kirafiki dhidi ya Iran, mchezo utakaopigwa Jumanne Machi 28, 2023.

Ukiwa ni mchezo wa kwanza kwa Kenya baada ya kuwa nje ya mashindano tangia Novemba 2021, kutokana na kufungiwa na Shirikisho la Kandanda duniani FIFA, kocha Engin Firat ameita majina ya wachezaji 24 pekee akiwa nahodha Olunga.

Jeuri ya kocha huyo eneo la kufumania nyavu imeangukia kwa nahodha Michael Olunga, Masud Juma na mshambuliaji anayekipiga Norwei Alfred Scriven.

“Hiyo siyo nafasi ya mwisho kwa Omala. Najua atakuwa na kesho nzuri ngazi ya klabu na taifa (Harambee Stars). Atafunga magoli tu, ila najua kila kocha anamahitaji yake na anataka mchezaji acheze vipi, lazima tukubali hilo”, alisema kocha McKinstry.

Author: Asifiwe Mbembela