Omanyala Avunja Rekodi ya Miaka 60, Ashinda Medali ya Dhahabu

163

Mfukuza upepo wa kimataifa wa Kenya Ferdinand Omanyala amefanikiwa kuvunja rekodi ya zaidi ya miaka 60 kwa kushinda medali ya dhahabu kwa Kenya katika mbio za mita 100 kwenye mashindano ya Jumuiya za Madola ambayo yanaendelea Jijini Birmingham, Uingereza.

Omanyala alitumia muda wa sekunde 10 nukta 02 ikiwa ni medali ya dhahabu ya kwanza kwa Kenya katika michuano hiyo inayoendelea hivi sasa, lakini inavunja rekodi iliyodumu kwa miaka zaidi ya 60.

Miongoni mwa waliokuwa washindani wa karibu ni Akani Simbine wa Afrika Kusini ambaye alitumia muda wa dakika 10 na sekunde 13 wakati Yupun Abeykoon raia wa Sri Lanka alitumia muda wa dakika 10 na sekunde 14.

Author: Bruce Amani