Onyango ang’aa Simba atwaa tuzo ya Mchezaji Bora wa Machi

Mlinzi wa kati wa Simba Joash ameshinda tuzo ya Mchezaji Bora wa Mashabiki wa mwezi Machi (Emirate Aluminium Simba Fans Player of the Month) ambayo imekuwa na utaratibu wa kutolewa na taasisi hiyo.

Onyango ambaye ni mchezaji wa zamani wa Gor Mahia alikuwa anashindana kupata tuzo na mshindi wa Mwezi Februari, kiungo Luis Miquissone ambaye alikuwa ameingia kwa mara nyingine tena kwenye mchakato wa kuisaka tuzo hiyo kwa mwezi Machi.

Pia nyota mwingine ambaye alikuwa kwenye mchakato wa kuwania tuzo hiyo ni kipa namba moja wa Simba, Aishi Manula.

Baada ya kura kupigwa kupitia mitandao, mashabiki ambao ndio wapigaji wa kura hizo wamempa ushindi beki wao Onyango ambaye leo amekabidhiwa tuzo yake.

Author: Asifiwe Mbembela

Sharing is caring!

0Shares