Orodha kamili ya mataifa yaliyofuzu katika CHAN 2020

Hatua ya kutafuta tiketi ya kufuzu michuano ya CHAN 2020 imekamilika rasmi kwa timu 16 kujikatia nafasi ya kushiriki mashindano hayo mwaka 2020 kuanzia mwezi Januari – mwezi wa pili nchini Cameroon.
Katika mchakato uliochukua kipindi kirefu mataifa makubwa kwenye soka la Afrika kama Misri, Ghana yameshindwa kupata tiketi baada ya kuondolewa katika hatua ya pili ama ya kwanza.  Upande wa Afrika Mashariki nchi tatu zitauwakilisha ukanda huo ambapo Uganda “The Cranes” ndiyo taifa lililoshiriki mashindano hayo mara nyingi 5, Tanzania mara 2 na Rwanda utakuwa mchuano wa nne kucheza.
Orodha yenyewe imekaa hivi:-
Cameroon (Wenyeji), Tanzania, Uganda, Zambia, Rwanda, Namibia, Togo, (Mara ya kwanza), Morocco, Zimbabwe, DR Congo, Congo, Tunisia.
Timu nyingine ni Burkina Faso, Guinea, Niger, na Mali.
Morocco ndiyo mabingwa watetezi wa michuano hii baada ya kufanikiwa kutwaa ubingwa wa huo mara ya mwisho mwaka 2018 wakiifunga Nigeria.
Michuano ya Chan huusisha wachezaji wanaocheza Ligi za ndani za mashirikisho husika, mfano mchezaji wa Tanzania anacheza klabu yoyote ya Tanzania anaruhusiwa kushiriki.

Author: Bruce Amani

Share With Your Friends