Pablo Martin aanza tambo Simba

Waswahili husema kipato huleta majivuno. Wengine huenda mbali na kusema pata tujue tabia yako.

Pengine ni baadhi ya kauli ambazo zinaangukia kuelezea kuwa mtu/binadamu akipata kitu ni rahisi kusema na siha yake kutambulika kiurahisi.

Kocha wa klabu ya Simba Pablo Martin akitetea na Waandishi wa Habari muda mfupi baada ya mtanange wa Ligi Kuu kumalizika kwa faida ya klabu yake na ushindi wa goli 3-1 ameonekana akitamba kikauli ambacho unaweza kutafsiri kama ni majivuni ya alama tatu.

Mabao ya Simba yamefungwa na Meddie Kagere goli mbili na Kibu Denis goli moja wakati bao la kufuatia machozi kwa Ruvu Shooting ambao walitamba sana kabla ya mchezo limewekwa kimiani na Elias Maguli.

Mchezo huo ambao ni wa kwanza kwa kocha huyo amesema ameridhishwa na matokeo hayo ambayo yatawapa vijana ujasiri wa kupambana katika michezo miwili ijayo dhidi ya Geita Gold, Yanga na michuano ya Kombe la Shirikisho Barani Afrika.

Licha ya ushindi huo Pablo amesema hakufurahishwa na namna vijana wake walivyocheza kipindi cha pili wakishindwa kupachika bao lolote na kuruhusu bao moja.

“Bila kujali idadi ya mabao huu ushindi ni muhimu kwetu kwa sababu utarejesha hali ya kujiamini kwa vijana bado tuna mechi ziko mbele yetu na zote tunahitaji kushinda,” amesema Pablo.

“Tuna michezo kama mitatu iko mbele yetu tunahitaji kufanyia kazi mapungufu lakini kiujumla nafurahishwa na wachezaji wangu wanavyowajibika uwanjani na kufanyia kazi yale tunayoyapanga japo bado safari ni ndefu lakini timu hii ina wachezaji wazuri,” amesema.

Matokeo hayo yanaifanya Simba kufikisha pointi 14 nyuma ya vinara Yanga wenye pointi 15 na mchezo mmoja mkononi utakaochezwa kesho w dhidi ya Namungo.

Author: Asifiwe Mbembela

Share With Your Friends