Pacquiao ana uhakika wa kuzichapa dhidi ya Broner

Mwanabondia kutoka Ufilipino Manny Pacquiao amesema pambano lake la mwezi Januari mwaka ujao dhidi ya Mmarekani Adrien Broner, litaendelea kama ilivyopangwa.

Hata hivyo, amekanusha ripoti kuwa huenda akapng ulingoni kwa pigano la marudiano dhidi ya mpinzani wake Floyd Mayweather. Pamoja na hilo amesema bado yupo ulingoni na hana mpango wa kustaafu hivi karibuni kama inavyoripotiwa. Pambano la Pacquiao na Broner litafanyika tarehe 12 au 19 mjini Las Vegas.

Author: Bruce Amani

Share With Your Friends