Palace yasitisha ushindi wa mfululizo wa Arsenal

53

Klabu ya Crystal Palace imetoshana nguvu na Arsenal baada ya penati mbili murua za nahodha wa timu hiyo Luka Milivojevic na magoli ya mawili kutoka kwa wachezaji wa Arsenal kuzipa timu hizo sare ya 2-2. Matokeo hayo yamefikisha mwisho ushindi mara 11 mfululizo wa Arsenal. Arsenal wamebaki katika nafasi ya nne nyuma ya Manchester City ambao wanaweza kuchukua usukani wa ligi kama watawashinda Tottenham Hotspur katika mchezo wa Jumatatu usiku

Mserbia Milivojevic alisawazishia Palace kupitia penalti baada ya goli lenye utata la Pierre-Emerick Aubameyang kuiweka Arsenal kifua mbele baada ya mapumziko.

Milivojevic alifunga goli katika kipindi cha kwanza baada ya Shkodran Mustafi kumwangusha Cheikhou Kouyate kwenye eneo la kumi na nane.

Granit Xhaka aliisawazishia Arsenal kwa faulo alipofunga freekick maridadi kabisa. Wilfried Zaha aliiangushwa na Xhaka katika boksi dakika saba kabla ya kumalizika mchezo na Milivojevic akafunga goli lake la pili kwa njia ya penati ambapo alimpeleka kushoto kulia kwa mlinda mlango wa Arsenal Bernd Leno.

Author: Bruce Amani