Paris Saint-Germain yashika usukani wa Ligue 1 kwa kutoa kichapo cha 4-0 Nimes

254

Baada ya kuanza vibaya kwenye mechi mbili za ufunguzi wa Ligue 1, Mabingwa watetezi wa Ligi Kuu nchini Ufaransa Paris St-Germain wameshikilia usukani wa ligi hiyo baada ya kutoa kichapo cha goli 4-0 dhidi ya Nimes. Mshambuliaji wa kimataifa wa Ufaransa Kylian Mbappe alifunga magoli mawili, beki wa kulia Alessandro Florenzi alitupia bao moja, na Pablo Sarabia aliweka kambani bao la mwisho.

Mlinzi wa Nimes Loick Landre alitupwa nje kwa kuonyeshwa kadi nyekundu baada ya kumfanyia faulo kiungo Rafinha.

Kiungo Rafinha, alijiunga na mabingwa hao wa Ufaransa kwa mkataba wa miaka mitatu akitokea Barcelona alikuwa kwenye kiwango bora ambapo alitoka na goli moja kabla ya kufanyiwa mabadiliko.

PSG walikuwa bila mchezaji muhimu Neymar, ambaye aliachwa kwenye kikosi baada ya kukitumikia kikosi cha timu ya taifa ya Brazil alipohusika kufunga goli tatu dhidi ya Peru mtanange uliopigwa Jumatano wa kufuzu Kombe la Dunia Qatar.

Fowadi wa Everton Moise Kean, aliyejiunga na PSG kwa mkopo alicheza mechi yake ya kwanza ndani ya uzi huo lakini haukuwa katika ubora wake.

Author: Bruce Amani