Pato Ngonyani, Kaheza watemwa jumla Polisi Tanzania

Kikosi cha timu ya Polisi Tanzania kimefikia maamuzi ya kuachana na wachezaji 13 kufuatia kumalizika kwa mikataba yao na sasa kuwa huru kuondoka na kwenda kwingineko kwenye msimu wa mashindano 2021/22, Pato Ngonyani ni miongoni mwa wachezaji ambao wametemwa.

 

Kupitia taarifa rasmi iliyotolewa Leo Jumanne Julai 20 na kitengo cha Habari na Mahusiano klabuni Polisi kimeweka idadi ya wachezaji na kuwatakia kila la kheri kwenye taaluma yao huko waendako.

 

Wachezaji ambao wametemwa wametajwa kuwa ni Marcel Kaheza, Mohhammed Bakari, Mohammed Yusuph, Mohammed Kassim, Ramadhan Kapele, Pato Ngonyani na Pius Buswita.

 

Wachezaji wengine ni Jimmy Shoji, Joseph Kimwaga, George Mpole, Emmanuel Manyanda, Erick Msagati na Hassan Nassoro.

 

Polisi Tanzania ambayo inanolewa na kocha Malale Hamsin “Care” imemaliza msimu wa 2020/21 ikishika nafasi ya sita na alama zao 45 wakiwa na hasara ya bao 2, nyuma ya KMC wenye alama 48 juu ya Tanzania Prisons wenye pointi 44.

Author: Asifiwe Mbembela

Sharing is caring!

0Shares