Pogba aisaidia Man United kuibomoa Bournemouth 4-1

180

Kocha wa Manchester United Ole Gunnar Solskaer alishuhudia timu yake ikisherehekea ushindi wa karamu ya mabao katika mechi yake ya tatu akiwa usukani, lakini amesema baada ya ushindi wao wa 4-1 dhidi ya Bournemouth kuwa kwa sasa lengo lake sio tu kucheza “kandanda la kushambulia zaidi”

United ilionyesha mchezo safi sana kaika kipindi cha kwanza na kufunga mabao matatu, ambapo Paul Pogba alifunga mawili kabla ya Marcus Rashford kufunga la tatu. Nathan Ake aliifungia Bournemouth kwa njia ya kichwa kabla ya Romelu Lukaku kuingia uwanjani na kufunga la nne.

United sasa wako katika nafasi ya sta, pointi tatu pekee nyuma ya nambari tano Arsenal. “kila mmoja anadhani kuwa nnataka tu kandanda la kushambulia zaidi kila wakati,” alisema Solskjaer. “Lakini msingi ni namna unavyojilinda na kutorufusu kufungwa bao na kisha utakuwa na nafasi nzuri ya kushinda mchezo wa kandanda.”

Manchester City warejea

Manchester City waliwazaba Southampton 3 – 1 na kupunguza pengo kati yao na vinara wa ligi Liverpool hadi pointi saba. David Silva aliifungia City bao la kwanza kabla ya wenyeji kusawazisha kupitia Pierre-Emile Hojbjerg. City walikuwa na bahati nzuri baada ya kombora la Raheem Sterling kumgonga James Ward-Prowse na kuingia wavuni kufanya mambo kuwa 2-1. Bao la kichwa la Sergio Aguero likawapa City pointi tatu

Chelsea yapata ushindi mgumu

Mapema Jumapili, Chelsea walipambana na Crystal Palace iliyowadhibiti katika mchezo ambao vijana hao wa Maurizio Sarri waliibuka na ushindi mwembamba wa 1-0 kupitia bao la NGolo Kante. Chelsea sasa wamejiimarisha katika nafasi ya nne na pengo la pointi tano dhidi ya Arsenal

Author: Bruce Amani