Pedri amwaga wino Barcelona

Kinda wa Hispania Pedri amekubali kuongeza mkataba mpya wa kuendelea kukitumikia kikosi hicho ambacho sasa kimeweka kipengele cha kuondoka klabuni hapo kwa dau la Euro bilioni 1 sawa na pauni milioni 846.

Pedri mwenye umri wa miaka 18, mkataba huo mpya utadumu mpaka Juni 30, 2026, ambapo anategemewa kumwaga wino rasmi kesho Ijumaa Octoba 15.
Pedri alijiunga na Barcelona kutokea Las Palmas Agosti 2020, amecheza jumla ya mechi 53 klabuni hapo tangia msimu uliopita, zikiwa ni mechi nyingi kuliko mwingine.
Ubora wa Pedri ulionekana pia kwenye michuano ya Euro 2020 ambapo alikisaidia kikosi cha Hispania kufika hatua ya nusu fainali.

Author: Asifiwe Mbembela

Share With Your Friends