Pep Guardiola amtamani Jack Grealish, Chelsea wamtaka Oliver Giroud kubakia Stamford Bridge

150

Kocha wa Manchester City Pep Guardiola anahitaji klabu hiyo imsajili kiungo mshambuliaji wa Aston Villa Jack Grealish, 25, katika majira ya kiangazi ikiwa ni sehemu ya kuboresha kikosi chake.

Kocha wa Manchester United Ole Gunnar Solskjaer amesisitiza kuwa mlinda mlango wake Dean Henderson, 23, anahitaji kuendelea kuitumikia klabu ya United licha ya kuibuka kwa tetesi za kuwa kipa huyo anataka kuihama timu hiyo Januari.

Licha ya fowadi wa Chelsea Oliver Giroud kutamani kuondoka klabuni hapo kocha wa klabu ya Chelsea Frank Lampard kusema bado anamhitaji kwenye kikosi cha Chelsea Stamford Bridge.

Chelsea wana matumaini ya strika wao Giroud atabakia Stamford Bridge licha ya matamanio ya mshambuliaji huyo.

Real Madrid hawajapokea ofa yoyote ile ya klabu ya kumhitaji kiungo mshambuliaji wa Hispania Isco, 28, awali alikuwa anahusishwa kutua Manchester City na Arsenal.

Author: Bruce Amani