Pep Guardiola amwaga wino mkataba mpya Manchester City

Kocha Mkuu wa kikosi cha Manchester City Pep Guardiola amefuta tetesi zilizokuwa zikimhusisha kujiunga na miamba ya soka la Hispania FC Barcelona kwa kusaini mkataba wa miaka mitatu ambao utamfanya kusalia klabuni hapo mpaka mwaka 2023.

Kocha huyo mwenye umri wa miaka 49, tayari ameshashinda taji la EPL mara mbili, Kombe la FA na taji la Kombe la Ligi tangu alipojiunga na City mwaka 2016.

Kocha huyo wa zamani wa Barcelona na Bayern Munich mkataba wake wa sasa ulikuwa unamalizika mwishoni mwa msimu huu ambapo sasa inakuwa mara ya kwanza kwa kocha huyo kukaa kwenye timu moja kwa kipindi kirefu cha miaka nane tangu ambapo alianza kufundisha soka mwaka 2008.

Kwa ujumla, Manchester City wameshinda mechi 181 katika mechi 245 chini ya Pep Guardiola na wana wastani wa kushinda mechi kwa asilimia 73.87.

Author: Bruce Amani