Pepe awapa Arsenal bao la ugenini wakati wakipoteza 2 – 1 dhidi ya Villarreal

Kikosi cha Arsenal kimekubali kipigo cha goli 2-1 kikiwa ugenini dhidi ya Villarreal kwenye mechi ya mkondo wa kwanza wa nusu fainali Ligi ya Europa iliyopigwa nchini Hispania Leo Alhamisi.

Katika mchezo huo uliokuwa na ushindani mkubwa kwa pande zote mbili, Arsenal walijikuta wakiwa pungufu kufuatia Dani Ceballos kuonyeshwa kadi nyekundu wakati wakiwa nyuma kwa bao 2-0.

Hata hivyo, winga wa Nicolas Pepe alikwamisha mpira nyavuni kwa njia ya penati baada ya kiungo mshambuliaji Bukayo Saka kufanyiwa adhabu.

Mchezaji wa Villarreal pia alionyeshwa kadi ya pili ya njano na hivyo kutimuliwa uwanjani. Matokeo hayo yanaifanya Arsenal kuwa na matumaini ya kufuzu kuingia hatua ya fainali kwa miaka mitatu kutokana na kuwa na goli la ugenini kuelekea mtanange wa marejeano.

Author: Asifiwe Mbembela

Sharing is caring!

0Shares